Profesa Chibunda: Utafiti ni nguzo ya maendeleo

CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA,) kitaendeleza mpango wa utoaji ruzuku ya fedha ili kusaidia watafiti wachanga wa ndani ya chuo ili kuinua na kukuza umahili wao na kuboresha miundombinu ya chuo hicho.

Katika kuendeleza mpango huo , chuo hicho kwa  mwaka wa fedha wa 2025/2026 kimetenga kiasi cha Sh bilioni 1.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Raphael Chibunda amesema kati kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli  kwenye hafla ya majalisi ya 42 ya ugawaji tuzo kwa wanafunzi na watumishi waliofanya vyema kitaaluma, utafiti na ubunifu katika chuo hicho.

“Mpango huu unalenga kuunga mkono  kuwa utafiti ni nguzo kuu ya kuendesha maendeleo ya taifa na ni muhimu kuweka msukumo katika suala hilo,” amesema Profesa Chibunda.

Katika hatua nyingine amesema chuo  kitaendelea kuzalisha wanafunzi mahiri  ambao wataweza kutumia elimu yao kujiajiri wao wenmyewe badala ya kusubiri kuajiliwa.

Profesa Chibunda pia amesema kupitia Mpango wa Jenga Kesho Bora (BBT), Chuo Kikuu hicho kilipewa jukumu la kusaili na kujaza nafasi 2,000 za wagani na miongoni mwao ni kwenye zao la pamba ,Korosho pamoja na parachichi.

“Taarifa tuliyonayo kutoka maeneo ya mazoezi ya vitendo ,wanafunzi hawa wamefanya vuziri na kuwezesha kuongezeka kwa uzalishaji utaotokana na wakulima waliofundishwa teknolojia za kisasa za kilimo,” amesema  Profesa Chibunda.

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam ,Profesa Maulid Mwatawala amesema  utaratibu wa kugawa tuzo  ni kawaida kwa  chuo hutoa  zawadi kwa wanafunzi na wanataaluma waliofanya vyema katika masomo na tafiti  kuwa ni kichocheo cha kuongeza ufanisi katika masomo, utafiti na ubunifu.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button