Rafiki Australia Tanzania yatoa taulo za kike Mafinga

IRINGA: Wasichana wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga wamepata faraja mpya baada ya Rafiki Australia Tanzania (Rafiki), kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi, na Wizara ya Afya, kuzindua mpango maalum wa kuwapatia taulo za kike za kisasa zinazoweza kutumika tena.
Katika uzinduzi uliofanyika Septemba 30, 2025, jumla ya Binti Packs 500 zilikabidhiwa kwa wasichana wa Shule ya Sekondari Kinyanambo na Shule ya Msingi Mkombwe.
Kila kifurushi kina taulo sita za kike zinazoweza kutumika kwa muda wa miaka miwili, kitabu cha elimu ya hedhi na kubalehe, pamoja na begi la kuhifadhia.
Takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa nchini Tanzania, wasichana wengi hukosa hadi asilimia 25 ya siku za masomo kila mwaka kutokana na changamoto ya kushindwa kudhibiti hedhi kwa usalama na heshima.
Wengi wao pia hawana elimu sahihi ya afya na usafi wa hedhi, hali inayowafanya kuishi kwa aibu, hofu na wakati mwingine kuacha shule kabisa.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Wizara ya Afya ilizindua mwaka huu Mwongozo wa Kitaifa wa Afya na Usafi wa Hedhi wa 2025.
Hatua ya Rafiki kuanzisha kampeni ya Rafiki wa Binti ni sehemu ya kuunga mkono jitihada hizo.
“Tunataka kuhakikisha msichana wa Kitanzania anabaki shuleni, anaendelea kusoma na kufikia ndoto zake bila kuzuiliwa na hedhi,” alisema Afisa Mradi, Saum Zidadu wakati wakikabidhi msaada huo kwa shule ya sekondari Kinyanambo.
Alisema tofauti na taulo za kibiashara zinazotumika mara moja na kutupwa, taulo hizi za kisasa zinazoletwa na Rafiki zinaweza kuoshwa na kutumika tena.
“Zimetengenezwa kwa vitambaa nyembamba vyenye uwezo mkubwa wa kufyonza, vinavyokauka haraka na salama kiafya. Pia ni rafiki kwa mazingira kwa sababu hupunguza taka ngumu zinazozalishwa na pedi za kutupa,” alisema.
Kwa mujibu wa wataalamu, taulo hizi zina uwezo wa kufyonza sawa na pedi nne za kawaida na zikihifadhiwa vizuri, hutoa huduma hadi miaka miwili.
Akikabidhi msaada huo alisema katika shule ya sekondari Kinyanambo, jumla ya paketi 395 zilitolewa, na kwa upande wa shule ya msingi Mkombwe nayo ilipokea paketi 105, na kufanya jumla ya msaada kufikia 500.
“Tunataka kuondoa kabisa kikwazo cha ukosefu wa vifaa vya kujisitiri, ili kila binti awe na nafasi sawa ya kusoma na kushindana darasani,” alisema Zidadu.
Mkuu wa shule ya sekondari Kinyanambo, Tumaini Mvile, alisema msaada huo utasaidia kuondoa changamoto za kisaikolojia na kiuchumi zilizokuwa zikiwakabili wasichana.
“Watakuwa huru kusoma kwa utulivu na kujiamini, bila woga wa kudharauliwa au kukosa masomo,” alisema.
Nao baadhi ya wanafunzi walioshuhudia tukio hilo walieleza furaha yao, wakisema awali walipata matatizo ya kiafya na hofu ya kudharauliwa kutokana na kutumia vifaa visivyo salama. Wamesema msaada huo utawawezesha kuongeza mahudhurio darasani na kuboresha ufaulu wao.
Kwa niaba ya Afisa Elimu Sekondari wa Mafinga, Lugelo Kambinda alisema mradi huo umekuja kwa wakati muafaka kwani umelenga familia zisizo na uwezo.
“Wengi walishindwa kumudu gharama za taulo, na matokeo yake walikosa masomo. Sasa tatizo hili linaanza kupungua,” alisema Kambinda.
Mradi wa Rafiki wa Binti tayari umetekelezwa Zanzibar na Karagwe kabla ya kuwasili Iringa, na matarajio ni kuendelea kusambaa nchi nzima, ili kuchochea mapinduzi ya kielimu kwa watoto wa kike nchini Tanzania.
Rafiki Australia Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na kusajiliwa nchini Australia na Tanzania. Kwa zaidi ya miaka 20 limekuwa mshirika muhimu wa Tanzania katika sekta za afya na elimu.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com