Rais anusurika kufa mara tano

MOGADISHU:RAIS wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, amesema kuwa yeye ndiye sasa shabaha kuu ya kundi la kigaidi la al-Shabaab linalohusishwa na mtandao wa Al-Qaeda.

Akizungumza katika mahojiano maalum na BBC, Rais Mohamud alifichua kuwa amenusurika majaribio ya mauaji mara tano ndani ya kipindi cha miaka miwili. “Wanaamini njia ya kusitisha vita dhidi yao ni kumuua rais,” alisema. Alibainisha kuwa ingawa miji mingi tayari imekombolewa, kundi hilo bado linaendelea kufanya shughuli katika maeneo ya vijijini.

Wachambuzi wa usalama pia wameonya  kuwa kundi la al-Shabaab linaendelea kuwa tishio kubwa, hasa katika maeneo ya kusini na katikati mwa Somalia. Aidha, Rais Mohamud alithibitisha uwepo wa wapiganaji wa kundi hilo waliovuka mpaka na kuingia Mandera, Kenya.

“Hatujafurahishwa na hilo. Tumejadiliana na serikali ya Kenya na wameahidi kuchukua hatua,” alisema na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika kulinda mipaka. SOMA: Rais wa Somalia anusurika shambulizi la bomu

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button