Rais Mwinyi : Kampeni za CCM zinaonesha taswira ya ushindi

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar , Dk. Hussein Ali Mwinyi leo tarehe  8 Septemba 2025 amekutana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dk. Asha Rose Migiro, Ikulu Zanzibar.

Dk. Mwinyi amempongeza Dk.Migiro kwa uteuzi wa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa na kueleza matumaini yake makubwa kutokana na uwezo wake, huku akifurahishwa na mwenendo wa kampeni za CCM unaoashiria kukubalika kwa Chama na ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Aidha, amemtakia mafanikio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa  Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM , Dk. Samia Suluhu Hassan, na kushukuru CCM Makao Makuu kwa msaada wake kuelekea uzinduzi wa Kampeni Zanzibar Septemba 13.

Naye, Katibu Mkuu Dk. Migiro ameahidi kushirikiana na CCM Zanzibar na kufanya kazi bega kwa bega katika kampeni. SOMA: Dk. Migiro: Tumewasha moto

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button