Rais Samia ataka udhibiti leseni za madereva
Vifo Arusha vyafikia 27, dereva wa Lori asakwa

RAIS Samia Suluhu Hassan ameviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama kudhibiti leseni za madereva wanaovunja sheria za barabarani.
Rais Samia ametoa agizo hilo kufuatia ajali iliyotolea Arusha jana Februari 24, 2024 majira ya saa 11 jioni watu 15 walipoteza maisha papo hapo na hadi kufikia leo jumla ya vifo 25 vimeripotiwa.
Katika salamu za pole, Rais Samia amesema “ajali zimechukua wapendwa wetu, nguvu kazi ya taifa na muhimili ya familia, naendelea kutoa wito kwa kila mmoja kuzingatia sheria za usalama barabarani katika matumizi ya vyombo vya moto.
“Naagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama na Kudhibiti kuendelea kuhakikisha vinasimamia kikamilifu sheria, ikiwemo ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya usafiri na kudhibiti leseni kwa madereva wanaorudia kuvunja sheria barabara na kusababisha watu kupoteza maisha, ” amesisitiza.
Nae, Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, CP Awadhi Juma Haji amesema idadi ya vifo vya ajali hiyo iliyotokea jana maeneo ya Ngaramtoni ikihusisha Lori na magari madogo matatu ni 25 kati yao wanaume 14, wanawake 10 na mtoto mmoja.
” Kati ya marehemu hao 25, saba ni raia wa kigeni waliokua wakijitolea kufundisha katika shule ya New Vision ambao walikua kwenye coaster ya shule hiyo,” amesema CP Awadhi.
Aidha, amesema hadi sasa majeruhi waliopo katika hospital ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru ni 21 wanaume 14 na wanawake saba.
Taarifa za awali zinasema chanzo cha ajali hiyo ni Lori kufeli breki na dereva alishindwa kulidhibiti.
Baada ya ajali hiyo dereva alikimbia, jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta dereva huyo aliyesababisha ajali hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.