Rais Samia awakumbuka JPM, Mwinyi, Lowassa

DODOMA; Rais Samia Suluhu Hassan, leo Juni 27, 2025, ameongoza taifa katika kutoa heshima kwa viongozi wakuu na wabunge waliotangulia mbele za haki tangu kuanza kwa Bunge la 12.

Akihutubia katika hafla ya kufunga rasmi Bunge hilo jijini Dodoma, Rais Samia aliwakumbuka kwa heshima kubwa Hayati Dk. John Pombe Magufuli (Rais wa Awamu ya Tano), Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi (Rais wa Awamu ya Pili), Mzee Cleopa David Msuya (aliyewahi kuwa Makamu wa Rais), na Mzee Edward Lowassa (Waziri Mkuu wa zamani).

“Ndugu viongozi, kama mnavyofahamu, tangu Bunge hili la 12 lianze, tumeondokewa na mpendwa wetu Hayati Dk. John Magufuli, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Cleopa David Msuya na Mzee Edward Lowassa,” alisema Rais Samia kwa sauti ya unyenyekevu.

Aidha, alikumbusha kuwa pia wapo wabunge waliokuwa sehemu ya Bunge hilo waliotangulia mbele za haki, akisema mchango wao hautasahaulika katika ujenzi wa taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button