Rais Samia Awateua Wabunge Sita

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameteua wabunge sita kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza leo Novemba 10.
Wabunge walioteuliwa ni Dk. Dorothy Gwajima, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Balozi Dk. Bashiru Ally, Abdullah Ali Mwinyi, Balozi Khamis Mussa Omar na Dk. Rhimo Nyansaho. SOMA: Rais Mwinyi atangaza mwelekeo mpya SMZ




Takwimu za mpaka mwishoni mwa mwaka 2020 zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR zinaonesha duniani kote kuna jumla ya wakimbizi milioni 82.4.
Takwimu hizi huenda zikaongezeka mwaka huu kwa kuwa janga la Corona au COVID-19 limesababisha watu wengi kuyakimbia makazi yao.
Nchi ya Syria ndio inaongoza kuwa na watu wengi chini ya himaya ya UNHCR ambako kuna jumla ya wakimbizi milioni 6.8, nchi inayofuata ni Venezuela ambayo ina jumla ya wakimbizi milioni 4.9.
Nchi nyingine mbili ni Afghanistan inayoshika nafasi ya tatu kwakuwa na idadi ya wakimbizi milioni 2.8 ikifuatiwa na taifa changa zaidi Afrika, nchi ya Sudan Kusini ambayo ina jumla ya wakimbizi milioni 2.2. Myanmara inashika nafasi ya 5 ikiwa na wakimbilizi Milioni 1.1 wanaosimamiwa na shirika hili la Umoja wa Mataifa
Na nchi inayoongoza kukaliwa na wakimbizi wengi ni Uturuki, ambayo imekaribisha takriban wakimbizi milioni 4, wengi wa wakimbizi hawa ni raia wa Syria ambao ni sawa na asilimia 92 ya wakimbizi wote nchini humo.
Nchi ya Colombia, taifa hili linahifadhi wakimbizi kutoka nchi mbalimbali lakini wanaoongoza kwa idadi kumbwa ni Venezuela ambao wako zaidi ya milioni 1.7.
Ujerumani inashika nafasi ya tatu duniani kwakuwa na idadi kubwa ya wakimbizi ambako takwimu zinaonesha jumla yao ni takriban milioni 1.5, katika nchi hii pia raia wa Syria pamoja na waomba hifadhi wanafikia asilimia 44 ya wakimbizi wote.
Mataifa yanayoshika namba 4 na 5 ni Pakistan na Uganda ambayo yamehifadhi jumla ya wakimbizi milioni 1.4 kila moja.
Wakimbizi Watoto
Takriban watoto milioni moja wamezaliwa nje ya mataifa yao kati ya mwaka 2018 na 2020, idadi hii ni sawa na uwiano wa watoto kati ya 290,000 na 340,000 kwa mwaka.
Suluhu ya kudumu kwa Wakimbizi
Pamoja na kuwapatia misaada mbalimbali UNHCR kwakushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa pamoja na wadau wake, wanaendesha programu mbalimbali zitakazowawezesha wakimbizi kupata suluhisho la kudumu
Kuwarejesha makwao:
Wakimbizi ambao walikimbia nchi yao kwasababu fulani mfano machafuko au baa la njaa na nchini mwao hali ikatengemaa husaidiwa katika mchakato wa kurejea makwao.
UNHCR haiwalazimishi wakimbizi hawa kurudi nyumbani bali ni maamuzi yanayofikiwa na wakimbizi wenyewe.
Ilihali mwaka 2020, nchi nyingi zilifunga mipaka yake kutokana na janga la Corona lakini jumla ya wakimbizi 251,000 walifanikiwa kurejea kwenye nchi zao za asili, idadi hii ni ya tatu kwa udogo katika kipindi cha muongo mmoja.
Watu milioni 117 wanaishi kama wakimbizi duniani
Rodrigo Menegat Schuinski
20.06.202420 Juni 2024
Leo ni maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani. Na kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa, watu wapatao milioni 117 walilazimika kuyakimbia makazi yao duniani kote kutokana na mizozo.
Kufikia mwishoni mwa mwaka 2023, kiasi cha watu milioni 117 duniani kote waliyakimbia makazi yao kutokana na mizozo, mateso au vitisho vingine dhidi ya maisha yao. Takwimu hizi ni kulingana na ripoti ya hivi karibuni kabisa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Kwa mujibu wa ripoti hiyo kiwango cha watu wanaogeuka wakimbizi kinaongezeka duniani
Kati ya wakimbizi milioni 117 duniani waliorodheshwa na UNHCR, milioni 68.3 walikuwa ni wakimbizi wa ndani, ikimaanisha kwamba walilazimika kuyakimbia makazi yao na jamii, lakini walisalia ndani ya mipaka ya nchi zao za asili.
Takwimu hizo za UNHCR zinahusu tu watu waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia na vita. Kituo kinachofuatilia wakimbizi wa ndani cha IDMC kinakadiria kuwa watu milioni 7.7 zaidi wamekuwa wakimbizi kutokana na majanga ya asili na mabadiliko ya tabia nchi.