Rais Samia: Dk Tulia haujatuangusha wanawake

DODOMA; Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, amempongeza Spika wa Bunge la la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk Tulia Ackson, kwa uongozi bora na usimamizi mahiri wa shughuli za Bunge la 12, akieleza amekuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake nchini.

Akihutubia Bunge leo Jun 27, 2025, Rais Samia ametoa pongezi hizo kwa Spika  Tulia kwa mafanikio makubwa katika kuongoza na kufanikisha mikutano yote 19 ya Bunge hilo hadi kukamilika kwake kwa ufanisi mkubwa.

“Najua haikuwa kazi rahisi, lakini ni kazi nyepesi kwako. Kwa uhodari mkubwa umeifikisha mashua yetu salama bandarini, kama manahodha makini wanavyofanya. Hakika haujatuangusha sisi wanawake wenzio,” amesema Rais Samia.

Amesema Dk. Tulia, akiwa mwanamke wa pili kushika nafasi hiyo ya juu katika muhimili wa Bunge, ameonesha weledi, uthubutu na kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yake ya kiuongozi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button