Rais Samia kinara mafanikio sekta ya nishati-Dk. Biteko

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameongoza kwa mafanikio makubwa katika sekta ya nishati nchini kwa kuzalisha umeme wa kutosha, huku ikihifadhi kiasi kikubwa cha umeme wa ziada.

 

Akimkaribisha Rais Samia kuhutubia kwenye Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika ‘Mission 300’ kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Dk. Biteko amesema katika kipindi chake (Rais Samia), kila kijiji nchini Tanzania kimefikishiwa umeme kupitia gridi ya taifa.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko

“Kwa juhudi zake, Tanzania imefanikiwa kuunganisha gridi yake ya umeme na nchi nne jirani, na hivi karibuni nchi nyingine mbili zitaunganishwa:

“Mara nyingi inasemwa kuwa mustakabali wa dunia uko mikononi mwa Afrika. Kauli hii inaweza kuhusishwa na wingi wa rasilimali za bara hili na idadi kubwa ya vijana waliopo, lakini pia ni ishara ya uongozi wa kimkakati na maono thabiti ya viongozi wa Afrika,” amesema waziri huyo wa nishati.

SOMA: Kauli za Dk Biteko ufunguzi mkutano wa nishati Afrika

Amesema, Rais Samia ni mfano halisi wa uongozi wa aina hii: “Tangu siku ya kwanza ya uongozi wake, amefanya kazi bila kuchoka kuhakikisha mahitaji ya nishati yanatimizwa, huku pia akihakikisha matarajio ya watu wake yanatimizwa.

 

Rais Samia pia ni kinara wa Mpango wa Upikaji Safi wa Tanzania, ambao ulijumuisha kuanzishwa kwa Mkakati wa Taifa wa Upikaji Safi,”

 

Naibu Waziri Mkuu, ameongeza kuwa katika jukwaa la kimataifa, Rais Samia, amekuwa mstari wa mbele kusukuma ajenda ya upikaji safi, ikiwemo uzinduzi wa Mpango wa Msaada wa Wanawake wa Afrika katika Upikaji Safi wakati wa Mkutano wa COP28 huko Dubai, kuongoza Mkutano wa Upikaji Safi huko Paris, na kushiriki katika miradi mingine mingi inayohusiana na nishati duniani.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button