RAIS Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kufungua mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki (EAMJA) utakaofanyika Arusha kuanzia Desemba 2 hadi 7 ,mwaka huu.
Lakini pia uboreshaji wa utoaji haki katika migogoro ya kazi ni mojawapo kati ya maeneo matano yatakayojadiliwa katika mkutano.
Akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ,Dk Gerald Ndika amesema mkutano huo wenye kauli mbiu ya ” Uboreshaji wa Mifumoya Utoaji Haki kwa ajili ya kuboresha utengamano na ukuzaji uchumi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAC)” utaangazia maeneo matano ambayo ni programu za maboresho ya mifumo ya utoaji haki jinai kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi wa utaoji haki jinai, program za utoaji haki katika mfumo wa madai ikiwemo mirathi, ajira, mikataba ikiwemo uboreshaji wa utoaji haki katika madai.
Eneo lingine ni uboreshaji wa utoaji haki katika migogoro ya kazi kwani migogoro ya kazi inahusu pia Baraza la ushulishi na ni eneo muhimu kwakua watu wengi wanajikuta wanaingia kwenye migogoro hiyo baina ya mwajiri na mwajiriwa na ikisimilizwa mapema inaongeza imani kwa wawekezaji na kuvutia wawekezaji katika ukanda wa EAC hususan katika sheria na maamuzi ya mahakama za juu kwa kila nchi yapoje ili kupata mwelekeo mzuri wa kutatua changamoto hizo
Pia matumizi ya teknolojia ya habari na masiliano katika utoaji haki kwani kwa upande wa Tanzania mahakama ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia (Tehama)na mawasiliano lakini pia watajifunza kwa nchi nyingine hatua walizofikia ambapo mkutano huo itashirikisha majaji na mahakimu zaidi ya 300.