Rais Samia: Madeni wakulima wa chai yatalipwa

MBEYA: Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali imeanza mchakato wa kuyachukua mashamba na viwanda vya chai ambavyo wawekezaji wake Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) na kampuni ya Wakulima Tea Company (WATCO) kutokana na kushindwa mikataba ya uwekezaji.

Pia amewahakikishia wakulima na waliokuwa wafanyakazi wa viwanda vya chai kuwa Serikali itasimamia kuhakikisha madeni yao wanalipwa.

Rais Samia ametoa ahadi hiyo leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika mji mdogo wa Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

“Serikali imeunda timu yankufanya tathimini ya viwanda na mashamba  ya chai, lengo letu ni tuyachukie na kuvipa vyama vya ushirika viendeshe chini ya usimamizi wa Serika. Kuhusu madeni tumeshazunguza na wawekezaji na tumewaunganisha na mabenki ili wakope na kuwalipa wakulima na wafanyakazi wa viwanda, niwahakikishe serikali itahakikisha mnalipwa.”

Kuhusu zao la parachichi Rais Samia alibainisha mikakati mikubwa ikiwamo yankujenga vituo 50 vya kuhifadhi parachichi kwa miezi mitatu ambavyo vitatumika ili kusubiri kupanda kwa bei katika soko la kimataifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button