Rasimu ya amani yawasilishwa DRC

DOHA : RASIMU ya makubaliano ya amani kati ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na waasi wa M23 imewasilishwa kwa pande husika, ikiwa ni sehemu ya mazungumzo yanayoendelea mjini Doha, Qatar.
Afisa anayehusika na upatanishi amesema pande zote mbili zimeonesha mwitikio chanya na kuonyesha utayari wa kuendelea na majadiliano, ingawa muda wa awali wa makubaliano haukufikiwa.,Serikali ya DRC na M23 tayari walisaini tamko la kanuni Julai 19 mwaka huu, wakilenga kufikia makubaliano ya amani Agosti 18.
Tangu 2021, M23 limefanikiwa kuteka maeneo makubwa kwa msaada wa Rwanda na kutawala miji muhimu ikiwamo Goma na Bukavu, hali ambayo imesababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu. SOMA: Rwanda, DRC waanza kutekeleza makubaliano ya amani