REA Kuzindua Mradi wa Umeme Mtera

SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatarajia kuzindua Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Mtera tarehe 16 Januari 2026, ikifuatiwa na kusaini mikataba 30 yenye thamani ya shilingi Trilioni 1.2 kwa ajili ya kusambaza umeme katika vitongoji 9,009 Tanzania Bara.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, amesema matukio haya yatafanyika Jijini Dodoma na yatashuhudiwa na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi. Kituo cha Mtera kimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 9.2 kwa ushirikiano na Serikali za Sweden na Norway. REA itafanya kazi na wakandarasi 21 wazawa na 9 kutoka nje ya nchi, wote wamesajiliwa nchini, kwa utekelezaji wa mradi wa miaka mitatu.

Mhandisi Saidy amewahimiza wananchi kuchangamkia fursa za ajira, biashara na huduma zitakazotolewa wakati wa utekelezaji wa mradi na kutumia umeme kuzalisha mali na kuboresha huduma za kijamii. “Mradi huu ni sehemu ya maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na ni mkubwa, kipekee na utasaidia kufungua nchi kiuchumi,” alisema Mhandisi Saidy. SOMA: REA kuhakikisha 80% wanatumia nishati safi 2034

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button