RSF yaunda serikali sambamba Sudan

KHARTOUM: KUNDI la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF) na washirika wake nchini Sudan wameunda serikali sambamba ya Muungano wa Tasis katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo.

Msemaji wa muungano huo, Alaa al-Din Naqd, ametangaza mamlaka hiyo mpya kupitia taarifa ya video kutoka mji wa Nyala, Darfur, unaodhibitiwa na RSF na washirika wake wa Janjaweed.

Muungano wa Tasis unaoongozwa na RSF umemteua Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, Kamanda wa RSF, kuwa Mkuu wa Baraza Kuu katika utawala huo mpya. SOMA: ICC yaonya mateso makali Sudan

Aidha, Mohammed Hassan al-Taishi, mwanasiasa wa kiraia ambaye alikuwa mwanachama wa Baraza la Mpito la Kijeshi na Kiraia lililotawala Sudan kufuatia kupinduliwa kwa Rais Omar al-Bashir mwaka 2019, ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa serikali hiyo.

Serikali hiyo sambamba imeundwa wakati mapigano kati ya RSF na Jeshi la Sudan yakiendelea, huku juhudi za kidiplomasia kurejesha amani zikisuasua.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button