Saa yatimia uteuzi wagombea ubunge CCM

DODOMA; MACHO na masikio ya Watanza nia leo yataangazia jijini Dodoma ambako Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaanza vikao vya kitaifa kuteua wanachama watakao peperusha bendera ya ubunge katika Uchagu zi Mkuu Oktoba 29, mwaka huu.

Vikao hivyo vinafanyika leo na kesho kutwa kwa ajili ya kuteua wanachama hao baada ya michakato kadhaa ya awali kukamilika katika ngazi mbalimbali za uteuzi kabla ya ngazi hii ya kitaifa.

Taarifa iliyotolewa Agosti 17, mwaka huu na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, ilisema vikao hivyo vitafanyika chini ya Mwenyekiti wa chama hicho Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, leo kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitafanyika kikifuatiwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Agosti 23, Agosti 2025.

Kwa mujibu wa Makalla, ajenda ya vikao hivyo itakuwa ni uteuzi wa wagombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wabunge wa viti maalumu. Pia vitateua wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi viti maalumu

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button