Samia asimamia miradi ya kimkakati

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi, amesema Rais Samia Suluhu Hassan amewaondoa hofu Watanzania kwa kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi ya kimkakati iliyoanzishwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.

Ameitaja baadhi ya miradi hiyo iliyoanzishwa na Rais Magufuli ikiwemo Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), reli ya kisasa (SGR) na ujenzi wa makao makuu ya serikali jijini Dodoma. SOMA: SGR Uvinza-Musongati, funguo muhimu milango mipya ya uchumi

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Sokoni, Mpwapwa Mjini mkoani Dodoma, Dk Nchimbi alisema wakati Rais Samia anaingia madarakani miaka minne na nusu iliyopita, Watanzania wengi walikuwa na mashaka na hofu kuhusu kama angeweza kuendeleza miradi hiyo mikubwa iliyokuwa bado katika hatua za awali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button