Samia ataja kilimo, nishati, viwanda Iringa

IRINGA: MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mgombea Urais wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema kipaumbele cha serikali atakayoiunda pindi akipewa ridhaa na wananchi ni kuimarisha nguzo kuu za uchumi, kilimo, nishati na viwanda ili kuhakikisha maendeleo yanamgusa kila Mtanzania.

Akizungumza kwenye kampeni za Uwanja wa CCM Samora mkoani Iringa, amesema, serikali yake tayari imekamilisha skimu ya umwagiliaji ya Sh bilioni 104.4 mkoani Iringa, ikinufaisha zaidi ya wakulima 62,800 na kuongeza tija ya kilimo, hivyo uzalishaji wa mahindi umefikia tani milioni 10 mwaka huu, hatua iliyoiweka Tanzania nafasi ya pili Afrika.

Amsema katika sekta ya kahawa, uzalishaji umeongezeka kutoka tani 109 mwaka 2021 hadi tani 323 mwaka huu, ongezeko linalowapa wakulima kipato na matumaini mapya.

Upande wa nishati, Rais Samia alisema uzalishaji wa umeme umeongezeka kutoka megawati 1,600 mwaka 2021 hadi megawati 5,000 mwaka huu, na lengo ni kufikia megawati 8,000, ili kuchochea viwanda na ajira.

Aidha, amesema viwanda mkoani Iringa vimeongezeka kutoka 24 hadi 40, hatua inayoongeza ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa ndani.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button