Samia ataka mapinduzi yalindwe kwa kutunza amani, mshikamano

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Mapinduzi ya Zanzibar ni kazi njema inayowaweka Watanzania kuwa wamoja, kuwainua kutoka hatua moja kwenda nyingine kimaende leo na kubadili hali ya maisha.

Rais Samia alisema hayo katika salamu zake za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi kwa Watanzania alizotoa kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Alisema Watanzania wana kazi ya kuendelea kuyalinda Mapinduzi kwa kuzitunza tunu za amani, umoja na mshikamano miongoni mwao.

“Nawatakia nyote heri ka tika Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Imekuwa miaka 61 ya kazi njema inayoendelea kutu fanya kuwa wamoja na bora zaidi.

“ Kazi ya kutuinua toka hatua moja kwenda nyingine kimaendeleo, kazi ya kubadili hali ya maisha ya wananchi wetu, na kazi ya kuendelea kuyalinda Mapinduzi kwa kuzitunza tunu za amani, umoja na mshikamano wetu,” aliandika Rais Samia.

Wakati huo huo, Rais Samia alihudhuria na kushiriki katika kilele cha sherehe za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani, Pemba. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko pia alishiriki katika sherehe hizo ambazo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi.

Habari Zifananazo

Back to top button