Samia kuongeza umeme 8000MW Namtumbo

NAMTUMBO : MGOMBEA wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kuongeza uzalishaji wa umeme hadi kufi kia megawati 8,000. Samia alisema hayo katika mkutano wa kampeni wilayani Namtumbo jana.
Alisema kwa sasa uzalishaji wa umeme umefikia megawati 4,000 na mpango wa miaka mitano ijayo ni kuongeza nishati hiyo hadi kufikia megawati 8,000 kwa kutumia vyanzo vya maji, jua, upepo na umeme wanyuklia kwa kutumia madini ya urani, yanayochimbwa Namtumbo.
Samia alisema utekelezaji wa mradi wa uchimbaji madini ya urani si tu utaongeza ajira kwa vijana lakini pia utaifanya Namtumbo kuchangia pato la taifa. Pia, ameahidi kutoa ekari 3,000 za Shamba la Mbegu za Kilimo (NAFCO) Namtumbo. SOMA: Kapinga ataja vigezo vya ziada upelekaji umeme vitongojini
kwa ajili ya wakulima. “Kulikuwa na kero kati ya wananchi na Hifadhi ya Shamba la Nafco Namtumbo. Tumelifanyia kazi na ekari 3,000 zitamegwa na kugawiwa kwa wakulima. Hivyo, wananchi watapata mashamba na Nafco itabaki na eneo kwa ajili ya kuendelea na kazi ya kuzalisha mbegu za kilimo na hasa ukizingatia tunataka kuondokana na utegemezi wa mbegu,” alisema Samia.
Alisema fedha zilizopelekwa katika wilaya hiyo pia zilitumika kuboresha huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo na kujenga vituo vya afya na zahanati, huku upatikanaji wa dawa ukifikia asilimia 80.
Aidha, Samia aliahidi kuendelea kuimarisha huduma za afya kwa kujenga vituo vya afya, zahanati, magari ya wagonjwa na kuimarisha huduma za rufaa ili huduma za kibingwa na ubingwa bobezi zipatikane ndani ya Mkoa wa Ruvuma.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com