‘Samia Legal Aid Campaign’ kuondoa msongamano magerezani

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk, Damas Ndumbaro amesema msaada wa kisheria unaotolewa na Rais Samia Hassan Suluhu wa ’Samia Legal Aid Campaign’ unalengo la kuondoa msongamano wa wafungwa na mahabusu kwenye magereza mbalimbali nchini.

Dk Ndumbaro amesema hayo leo alipotembelea Gereza Kuu Ausha lilipo Kisongo jijini Arusha kwa lengo la kuongea na wafungwa, mahabusu ili kujua changamoto zao  katika kupata msaada wa kisheria.

Amesema lengo la ziara hiyo ni kuwaeleza wafungwa hao na mahabusu waliopo gerezani kuwa Rais Samia ametoa msaada wa kisheria ili kuondoa msongamano magerezani  na kuwataka wafungwa hao kuonyesha nidhamu ikiwemo mahabusu kupata haki zao za kisheria kupitia kesi zinaoendeshwa mahakamani.

Advertisement

Amesema Rais Samia ameleta msaada huo wa kisheria usiobagua kwalengo la wafungwa/ mahabusu kunufaika nao kwa waliokata rufaa ikiwemo mahabusu ambao kesi zao zinaendelea kusikilizwa ili waweze kunufaika

“Tunaangalia mfumo wa haki jinai kupitia taasisi zetu ili zifungamane na taasisi za magereza kwa lengo la kusaidia wafungwa na mahabusu kupata haki ikiwemo kukata rufaa hivyo kampeni ya msaada wa kisheria ya Samia Legal Aid Campaign inasaidia wananchi kupata haki zao katika mkondo wa sheria”

Naye Kamishna wa Magareza (CP) Nicodemus Tenga ameshukuru ujio wa ziara ya Waziri Ndumbaro kwa lengo la kuangalia utoaji haki jinai ili kupunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu magerezani.