Samia: Madini ya urani ni hazina

RUVUMA: RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema uzinduzi wa kiwanda cha majaribio cha uchenjuaji wa madini ya urani kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma, ni hatua muhimu na ya kihistoria katika safari ya taifa kuelekea uchumi wa kisasa unaotegemea maarifa na rasilimali za ndani.

Akizungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi huo leo Julai 30 Rais Samia amesema moyo wake umejaa furaha, matumaini na imani kubwa kuwa Tanzania sasa imefungua ukurasa mpya wa kutumia madini ya urani kwa manufaa ya taifa.

Ameeleza kuwa madini ya urani ni miongoni mwa madini ya kimkakati duniani yanayotumika kuzalisha nishati ya nyuklia, tiba za saratani, na tafiti za hali ya juu za kisayansi, na kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zilizobarikiwa kuwa na akiba kubwa ya madini hayo.

Kwa mujibu wa taarifa za kiufundi, maeneo ya Mto Mkuju mkoani Ruvuma yanakadiriwa kuwa na uwezo wa kuzalisha hadi tani 300,000 za urani kwa mwaka, jambo linaloliweka taifa katika nafasi ya kipekee kwenye sekta hiyo.

Kiwanda hicho cha majaribio kimejengwa chini ya kampuni ya Mantra Tanzania Ltd, na kinatarajiwa kuwa msingi wa kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha kudumu cha uchenjuaji wa urani kwa matumizi ya ndani na kuuza nje.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button