Samia: Uhuru wa maoni umeongezeka Tanzania

DODOMA :RAIS wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amesema uhuru wa habari na watu kutoa maoni yao umeongezeka tofauti na hapo awali, kwani serikali imetoa leseni kwa magazeti na majarida 356,vituo vya redio 247,vituo vya televisheni 68 ,redio na televisheni za mtandaoni 325 na blogu 72.
Hayo ameyesema leo jijini Dodoma wakati akifunga bunge la 12 na kuongezea kuwa kwa sasa habari ipo kiganjani hivyo hakuna budi kuendana na teknolojia
“Serikali haijafanya uhakiki wa habari kabla ya kuandikwa na kuchapishwa tunafanya hivi kwa kuamini kwamba waandaji wa maudhui haya ni watu wenye ueledi wa kutosha na kwamba tunafanya ustawi wa demokrasia yetu hutegemea sana uhuru wa vyombo vya habari.
“Tunathamini na kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuelimisha jamii kupambana na maovu pamoja na kuhimiza uwajibikaji katika kulinda na kutambua michango ya waandishi wa habari kwa jamii tulifanya marekebisho ya sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 na kanuni zake pia tuliandaa tuzo za Samia Kalamu Awards kutambua waandishi wa habari za maendeleo Tanzania, ” amesema Rais Samia
Amesema serikalia haikusita kuchua sheria pale ambapo uhuru huo wa vyombo vya habari ulipotumika vibaya kwa kutishia kuleta vurugu nchini pamoja na kuvuruga usalama wa jamii.