Samia awakumbuke wanamitindo Tanzania

SERIKALI imetakiwa kulitupia jicho sekta ya mitindo nchini kwa kuipa kipaumbele na sapoti sawa na inavyofanya kwenye sekta ya michezo, hasa kwa wachezaji wa mpira wanapofunga magoli.

Akizungumza na HabariLeo, Msemaji wa Tanzania Fashion Festival (TAFF), Bhoke Egina, alisema lengo ni kuona sekta ya ubunifu inapata mashindano, pongezi na umaarufu sawa na ule wa michezo ili kukuza ajira na ubunifu wa vijana.

“Tunataka ushindani uliopo kwenye mpira uingie pia kwenye sekta ya ubunifu. Jukwaa la mitindo liwe kubwa zaidi, na wabunifu wetu washiriki kwenye matamasha makubwa duniani kama Marekani, Ufaransa na nchi zingine zilizoendelea,” amesema Bhoke.

Bhoke aliongeza kuwa mwaka huu tamasha hilo limevunja utamaduni wa zamani kwa kuwatumia wanamitindo wenye maumbo halisi ya Kiafrika, badala ya kuendelea na dhana kwamba mitindo ni ya watu wembamba pekee. SOMA: Sauti ya Mitindo yanogesha Miss Universe 2025

“Kwa muda mrefu tasnia ya mitindo imehusishwa zaidi na wasichana warefu wembamba, lakini safari hii tumeamua kuonesha kuwa hata wanawake na wanaume wenye maumbo ya Kibantu wanaweza kuonekana vizuri katika mavazi ya kisasa,” amefafanua.

Amesema pia jina la Hamisa Mobetto liliibuka kwa ajili ya kufungua tamasha hilo kutokana na mvuto wake wa Kiafrika, umaarufu na mchango mkubwa alioutoa katika sekta ya mitindo. “Hamisa ana mvuto wa kipekee, umbo la Kibantu na huvaa mavazi ya mitindo kwa ufanisi mkubwa. Kwa sasa tunaweza kusema ameliteka soko la mitindo Tanzania,” amesema Bhoke.

Bhoke ameongeza kuwa lengo kuu la tamasha hilo ni kutoa nafasi kwa wabunifu chipukizi na nguli wa mitindo kuonesha vipaji vyao, sambamba na kupinga dhana potofu kwamba mitindo ni ya watu wembamba pekee.

Mbali na Hamisa, wasanii wengine waliotajwa kuchangia kukuza sekta ya mitindo ni pamoja na Jux, Phina na Nandy, ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza ubunifu wa mavazi nchini. Aidha, Bhoke ametoa wito kwa kampuni na taasisi mbalimbali kujitokeza kudhamini matamasha ya mitindo ili kuendeleza vipaji vilivyopo na kuongeza fursa za ajira.

Usiku huo wa Tanzania Fashion Festival ulipambwa na muonekano wa Hamisa Mobetto na burudani kutoka kwa Barnabas Classic, huku ukifanyika katika ukumbi wa Delta Hotel, Masaki jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa wabunifu waliopata nafasi ya kuonesha mavazi yao ni Hamisa Mobetto, Agusta Masaki, Whyz Fashion kutoka Zanzibar, pamoja na wanamitindo wengine wengi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button