Senyamule apongeza NGOs kuchangia maendeleo ya mkoa

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amezipongeza Asasi Zisizo za Kiserikali (NGOs) mkoani humo kwa kutoa mchango wake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya mkoa huo, kwani zimeshiriki kikamilifu kujenga shule, kufadhili miradi na kujazia juhudi za serikali.
Akizungumza na wawakilishi wa NGOs mkoani hapo wakati akifungua kikaokazi na wadau hao, katika utaratibu wake wa kawaida wa kukutana na makundi mbalimbali kwa ajili ya kupanga mikakati ya maendeleo ya mkoa, amepongeza mchango wa NGOs katika maendeleo ya mkoa huo.
SOMA: Dodoma kuzindua kitabu cha kukuza utalii
Senyamule amesema NGOs zimekuwa zikisaidia katika shughuli nyingi, mfano katika ujenzi wa shule na katika miradi mingine. Jitihada hizo zimechangia katika kusaidia nguvu ya serikali katika kuboresha huduma za jamii.
“Tunaposhuhudia miradi ikikabidhiwa ambayo imejengwa na NGOS, ni wazi mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo kati ya serikali na hao washirika wa maendeleo,” amesema.
Pia, Senyamule ameizitaka NGOs hizo kujua vipaumbele vya maendeleo ya Mkoa wa Dodoma, ambavyo vipo vitano kikiwemo cha kilimo, utalii, kituo cha usafiri na usafirishaji, ujenzi wa viwanda na madini.
Alieleza kwamba, NGOs zinatakiwa kuingia kwenye malengo ya sekta ambazo zinagusa maisha ya watu katika vijiji kwa ajili ya kuinua uchumi wa mkoa.
Naye Ofisa wa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma, Honaratha Rwegasira amesema NGOs zimekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha mambo ya jamii, uchumi na utawala bora katika kufanya kazi kwa ukaribu na serikali za mitaa.
Honaratha alisema mkoa huo kwa sasa una NGOs hai 437 kati ya 527 zilizosajiliwa lakini pia 188 zilisimamishwa shughuli zake na 150 zilifutwa usajili wake kwa sababu mbalimbali.
Honoratha amesema NGOs mkoani humo zinafanya kazi katika sekta mbalimbali zikiwemo za afya, uchumi, haki
za binadamu, utawala bora, mazingira, kilimo, usawa wa kijinsia na maendeleo ya vijana.
Katika kipindi cha miaka mitano, NGOs zimechangia Sh bilioni 65.9 kwenye miradi iliyotekelezwa mkoani humo katika kuboresha elimu, afya, uwajibikaji na ustawi wa jamii katika mkoa.
“NGOs zimekuwa nguzo muhimu katika kuleta matokeo chanya katika jamii kwa kuzalisha fursa mbalimbali, kutatua changamoto na kujazilia juhudi za serikali,” amesema.
Naye mwakilishi kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake
na Makundi Maalumu, Dennis Mashaka amezikumbusha NGOs kutoa huduma ndani ya mamlaka na kuangalia
shughuli zao kama walivyosajiliwa, hasa kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.
…………… Audhuria graduation ya mwanaye
……………… Akutana na Dada yake aliyepotezana Naye Miaka 100 na kuambiwa anapenda story za ndoa
………….. Atembelewa na mcheza mieleka Maarufu duniani na wakala nyama ya ng’uruwe pamoja
……………. Akitana na mfanyakazi mwenzake wa jinsia tofauti barabarani na Kuoneshwa kitabu cha kumbukumbu
Akutana na mfanyakazi mwenzake wa jinsia tofauti barabarani na Kuoneshwa kitabu cha kumbukumbu
Akutana na kiongozi wake na kumwambia “Mwanao na wewe Ndio mnatakiwa kutuletea aina ya umalaya mathalani………….
……………. Atembelea chuo chake alichosoma bila nguo wenzake waamua kumpatia nguo ambazo hazistahili matako