Serikali kuendelea kudumisha demokrasia

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema serikali itaendelea kudumisha demokrasia nchini kwa kuyafanyia kazi mapendekezo na michango mbalimbali inayotolewa na vyama vya siasa, viongozi wa dini na asasi za kiraia kwa ustawi wa demokrasia.
Dk Mwinyi ameyasema hayo leo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati akifunga mkutano wa kitaifa wa wadau kujadili hali ya demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa serikali za vijiji, mtaa na vtongoji mwaka 2024 na uchaguzi mkuu mwaka 2025 lililofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Dk Mwinyi amezindua mradi wa kuimarisha mazungumzo ya vyama vingi vya siasa na kukuza ushirikishi wa Wanawake na Vijana katika michakato ya kisiasa na chaguzi nchini.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi
Una maoni usisite kutuandikia



