Serikali kuendelea kutekeleza afua za mpango shule salama

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) zimeanza utoaji mafunzo kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Shule Salama kwa walimu wanasihi  5,000 wa shule za awali na msingi nchini.

Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo, Dk  Charles Mahera amesema hayo wakati akifungua ngazi ya kitaifa mafunzo hayo kwa walimu wanasihi kwenye  Chuo cha Ualimu Morogoro.

Amesema katika utekelezaji wa mpango huo Walimu Wanasihi hao kutoka wa Shule za Msingi  5,000 zilizoteuliwa kutekeleza Afua ya Mpango huo kupitia Program ya BOOST kutoka halmashauri zote na mikoa  ya Tanzania Bara kuwa watajengewa uwezo.

Dk Mahera amesema mafunzo hayo yanalenga kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali zinazojitokeza zinakabiliwa ili mazingira ya utoaji wa elimu yanakuwa salama kwa ajili ya kuwasaidia walimu na wanafunzi kufikia malengo yao.

Ametaja maeneo muhimu  kati ya nane  yaliyowekewa umuhimu ni na namna kuimarisha utoaji wa huduma ya ushauri na unasihi shuleni, jinsi ya kukuza stadi za maisha za wanafunzi, jinsi ya kutatua na kushughulikia malalamiko mbalimbali ya walimu na wanafunzi.

Dk Mahera ametaja eneo lingine ni namna ya kubaini na kushughulika wanafunzi walio katika hatari ya kuacha shule, namna ya kubaini na kushughulikia mapitio hatarishi kwa wanafunzi kutoka nyumbani kwenda shule na kurudi nyumbani.

Pia namna  ya kuboresha utendaji kazi na kuzingatia maadili katika kazi ya ualimu, namna kuboresha na kuimarisha mahusiano kati ya Shule na jamii ikiwemo wazazi kupitia ushirikiano wa Wazazi na Shule.

Dk Mahera ametaja eneo lingine ni  jinsi ya kushughulikia na kutatua unyanyasaji wa kijinsia; na  jinsi ya kushirikiana na jamii kuhakikisha huduma ya chakula na lishe inatolewa shuleni.

Amesema serikali imetumia gharama kubwa kuwezesha mafunzo hayo  na hivyo kutaka yakawe chachu ya kuleta tija na thamani kwa fedha zilizotumiwa  kwa  kuhakikisha mazingira ya shule  yanaboreshwa ili kuwa salama kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji ulio fanisi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu Msingi wa wizara hiyo,  Abdul  Maulid amesema mafunzo hayo kwa baadhi ya walimu yamefanyika na mengine yanaendelea kufanyika  kwenye  vituo vitano tofauti ambavyo ni Chuo cha Ualimu Klerruu, Chuo cha Ualimu Morogoro, Chuo cha Ualimu Korogwe na Chuo cha Ualimu Tabora

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button