Serikali kuimarisha vitendea kazi bandari Mtwara

SERIKALI imesema itaendela kuleta vitendea kazi katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) mkoani Mtwara ili kuhakikisha ufanisi wa bandari hiyo unaongezeka.
Akizungumza leo mkoani Mtwara, Waziri wa Uchukuzi Profesa, Makame Mbarawa amesema mambo hayo yote Rais Samia Suluhu Hassan anayafanya ili kuhakikisha wanaongeza ufanisi wa bandari ya mtwara ili iweze kufanya kazi vizuri zaidi kuliko hapo awali.
Lengo la ziara hiyo ikiwa ni pamoja na kuja kuangalia hali ya usafirishaji wa zao la korosho katika msimu ya kilimo wa mwaka 2024/2025 unavyoendelea bandarini hapo pamoja na baadhi ya changamoto za kiutendaji bandarini hapo ili kama zipo ziweze kufanyiwa kazi na mengine.
‘’Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya ya kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye nchi yetu hasa kwetu sisi watu wa bandari, amekuwa akitupa msukumo mkubwa kuhusu usimamizi wa sekta ya bandari hapa nchini kuanzia kwenye usimamizi wenyewe na ujenzi wa miundombinu,” amesema Mbarawa.

Amesema matokeo ya jitihada hizo kwa sasa yanaonekana kwani mwaka mmoja uliyopita bandari hiyo walikuwa wanakuta meli moja kwa siku lakini sasa wanakuta meli mbili kwa siku ikiwa zinapakia korosho ghafi kwani hayo ni mabadiliko makubwa kwenye bandari hiyo.
Aidha mabadiliko hayo yamekuja kutokana na maoni ya Rais huyo kwasababu sasa vitendea kazi vimeongezeka bandarini hapo kwani zamani kulikuwa na vitendea kazi vichache huku akiwataka watendaji wa bandari hiyo kuwa waongeze ufanisi mkubwa katika utendeaji wa kazi wao ili kuleta tija ya kiutendaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amepongeza uwekezaji mkubwa unaofanywa wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika bandari ya Mtwara kwani uhudumiaji wa shehena umeongezeka bandarini hapo kupitia bidhaa mbalimbali ikiwemo zao la korosho.
Aidha kwa zao la korosho pekee mpaka sasa zaidi ya tani 100,000 za korosho ghafi zimesafirishwa kwenda nchi mbalimbali kupitia bandari hiyo.

Hata hivyo wananchi mkoani humo wanaendelea kunufaika moja kwa moja na uwepo wa bandari hiyo mbali ya mapato lakini wananufanika na suala la ajira bandarini hapo na kupelekea kukuza uchumi na familia zao.
Aidha amempogeza waziri huyo wa uchukuzi kwa usimamizi na ufatiliaji mzuri katika sekta hiyo kwani jitihada zake zinaonekana hasa utekelezaji wa maagizo ya Rais kuhusu korosho zote zinazozalishwa kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma zisafirishwe kupitia bandari hiyo.



