Serikali kuipa nguvu sheria uwezeshaji wazawa sekta madini

SERIKALI imeeleza kuwa imejizatiti kuongeza nguvu ya usimamizi thabiti wa sheria ya uwezesahji wazawa (Local Contents) kwa kuifugamanisha moja kwa moja sekta ya madini na sekta ya viwanda.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini, Janeth Lekashingo ametoa kauli hiyo katika kongamano maalum na wadau wa sekta ya madini katika Maonyesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mjini Geita.

Janeth amesema serikali inatambua kuwa tangu kuanza utekelezajiwa sharia ya Local Contents yamekuwepo mafanikio makubwa lakini matamanio ni kuona watanzania wanaendelea kupata fursa zaidi.

Amesema dhumini kuu ni ushirikishaji wa watanzania katika fursa zilizopo migodini ambao utaongeza kipaumbele kwenye faida za kiuchumi kwenye jamii katika sekta ya madini.

Amesema hatua hiyo inatokana na darasa iliyopata Tanzania kutoka nchi nyingi zenye utajiri wa madini barani Afrika ambazo zilijikita kukusanya kodi na tozo ambazo zilifikia kikomo baada ya uchimbaji kuisha.

Amesema kupitia ‘local Contents’ serikali inahakikisha watanzania wananufaika na fursa za madini na kupelekea kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, kampuni za watanzania na uchumi wa nchi kwa ujumla.

“Ushirikishaji wa watanzania unasaidia kufungamanisha sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi, na kampeni yetu mwaka huu (2025) ni kuungana na sekta ya viwanda” amesema.

Amekiri kuwa mpaka sasa wamiliki wengi wa leseni wameshaitikia sheria ya uhirikishaji wazawa kupitia fursa za ajira, manunuzi ya bidhaa za ndani, mafunzo, urithishaji ujuzi na maarifa.

“Tume ya madini inaendelea kufanya tathimini ili kujua hali halisi ya ushiriki wa watanzania katika fursa zilizopo migodini”, amesema Janeth.

Kamishna wa Tume ya Madini, Mhandisi Theonestina Mwasha.

Kamishna wa Tume ya Madini, Mhandisi Theonestina Mwasha amesema ili kuwezesha ushirikishaji timilifu wa watanzania tume inaendelea kufanya makongamano ili kutoa elimu ya wazi kwa wazabuni wazawa.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati amesema kampuni za migodi kutekeleza ushirikishaji wazawa inaongeza mnyororo wa thamani na hivo kupandisha kiwango cha ukusanyaji mapato serikalini.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Wanawake Nchini (TAWOMA), Salma Ernest ameiomba serikali kuendelea kuweka sera wezeshi kwa wachimbaji kukua zaidi na wawekezaji wazawa kuendelea.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button