Serikali kulipa mishahara wafanyakazi 473 halmashauri

ARUSHA: Makamu wa Rais Dk Philip Mpango ameeleza kuwa Serikali imeamua kulipa mishahara ya Watumishi 473 kutoka Halmashauri 101 kutokana na hamshauri hizo kushindwa kulipa mishahara hiyo kupitia mapato ya ndani.
Akizungumza leo katika Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yanayofanyika kitaifa mkoani Arusha Dk Mpango amesema zaidi ya Sh billion 3.5 zimetengwa kuzipiga jeki halmashauri hizo.
“Kuanzia mwezi Julai 2024, jumla ya Wafanyakazi 473 kutoka Halmshauri 101, watalipwa kupitia Mfuko Mkuu Serikali ambao ni zaidi ya Sh bilioni 3.5,” amesema Dk Mpango.
Katika hatua nyingine Dk Mapngo amezitaka halmashauri zote nchini kubuni vyanzo vya mapato ili kuipunguzia mzigo Serikali.