Serikali kuwaunga mkono wadau nishati safi

DAR ES SALAAM: Serikali imesema itaendelea kuwaunga mkono wadau katika kufanikisha lengo la serikali kwa wananchi kutumia nishati safi ili kuachana na kutumia nishati chafu kwani ina madhara kiafya.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia Kutoka Wizara ya Nishati, Nolasco Mlay wakati wa uzinduzi wa mradi wa nishati safi ya kupikia unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Waitaliano (CEFA).

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Kitaliano la (CEFA) nchini Tanzania Cinzia D’intino na Mtaalam wa Teknokojia ya Nishati Safi ya Kupikia, Saada Zaheer wamesema mradi huo unatumia umeme kidogo na utadumu kwa tanzania takribani miaka miwili na kuanzia watatoa majiko 50,000 kwa awamu ya kwanza na mbeleni watatoa majiko 150,000.

Wananchi walionufaika na mradi huo Tendeni Ally na Stapon Shayo wamesema nishati safi ya kupikia inawasaidia ukilinganisha na kipindi cha nyuma walivyokuwa wanatumia nishati chafu hivyo ilikuwa inachafua mazingira.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Jobathome1.Com