Serikali kuweka nguvu sekta ya elimu

SERIKALI  imesema itaendelea kuchukua hatua kuboresha utoaji elimu katika maeneo ya jumla na ya amali ili kuwezesha wadhibiti ubora wa shule na kubuni mbinu mbalimbali zitakazowezesha wanafunzi kuwa na ujuzi ikiwemo fursa za kujiajiri pasipo subiri kuajiriwa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 1, 2024 na Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Ubora wa Shule kutoka Wizara ya Elimu, Ephraim Simbeye wakati akizungumza kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu kutoka hiyo, Dk Charles Mahera katika mafunzo ya Wadhibiti Ubora wa Shule za Msingi na Sekondari 340 pamoja na waratibu wa mikoa kutoka WyEST kutoka mikoa 26 nchini.

Amesema mafunzo ya amali  yanalenga kuboresha elimu nchini ikiwemo mazingira ya kufundishia na kujifunza ili kupata matokeo chanya ya ujifunzaji hususan kwa wanafunzi.

Mikakati mbalimbali imewekwa na serikali katika kuhakikisha wanatumia mbinu za kuhamasisha washiriki kwenye ushiriki wa jamii ikiwemo kuleta maendeleo shuleni , kufanya ufuatiliaji na tathimini ya udhibiti ubora wa shule wa ndani.

“Mafunzo ya amali yatasaidia wanafunzi kupata fursa za kujikwamua kiuchumi ikiwemo kufikia Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025 pamoja na ajenda ya maendeleo endelevu ifikapo 2030 ,hivyo maofisa udhibiti ubora shirikianeni na walimu wengine shuleni ili kuleta tija zaidi”

Naye  Kamishna wa Elimu, Dk Lyambwene Mtahabwa amesema mafunzo hayo yanalengo la kuweka  mpangilio mzuri wa kazi ikiwemo kufundisha na wengine kazini mbinu  ufindishaji ili kuleta matokeo chanya katika kusimamia utoaji wa elimu bora.

Habari Zifananazo

Back to top button