Serikali sasa yamiliki kiwanda cha TBPL asilimia 100

DODOMA; WAZIRI wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema Serikali sasa inamiliki kwa asilimia 100 kiwanda cha Teknolojia ya Kutengeneza viuadudu (TBPL) kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.

Ametoa kauli hiyo leo, alipokuwa akichangia kwenye mdahalo wa uchambuzi wa bajeti kwa wabunge, ambapo baadhi ya wabunge waliulizia kuhusu kiwanda hicho hasa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Amesema tayari wameshamalizana na wenzao wa Cuba kuhusu kiwanda hicho na ndiyo sababu kwenye bajeti ya mwaka 2025/26 ya Tamisemi, wametenga bajeti kila halmashauri kwenda kununua dawa kwenye kiwanda hicho kutokana na maelekezo ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button