Serikali yatangaza mapumziko Oktoba 29

RAIS Samia Suluhu Hassan ameidhinisha Oktoba 29, 2025 kuwa siku ya mapumziko ili kuwawezesha wananchi wenye sifa stahiki wakiwemo watumishi wa umma na wafanyakazi wa sekta binafsi kupiga kura.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk Moses Kusiluka, hatua hiyo ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Rais chini ya Sheria ya Sikukuu za Kitaifa Sura ya 35.
Katika taarifa hiyo, Balozi Dk Kusiluka amesema Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza Oktoba 29, 2025 kuwa ni siku ya kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.
“Rais Samia kwa mamlaka aliyonayo ameidhinisha Oktoba 29, 2025 kuwa siku ya mapumziko,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
SOMA: Uchaguzi Mkuu Oktoba 29
Awali, INEC ilitoa ratiba ya kampeni za uchaguzi zilizoanza Agosti 28 na zin- azotarajiwa kuisha Oktoba 28, mwaka huu ili kupisha kura ya mapema na Oktoba 29 itakuwa siku ya Uchaguzi Mkuu.
Katika hilo, Agosti 27, mwaka huu INEC ilitangaza uteuzi wa wagombea 34 wa kiti cha rais na makamu wa rais kutoka vyama 17 vya siasa vilivyochukua fomu za uteuzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu.
Wagombea walioteuliwa ni Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Kiti cha Rais na Dk Emmanuel Nchimbi (Makamu wa Rais) kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wengine ni Hassan Almas (Urais) na Hamisi Hassan (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha National Recon- struction Alliance (NRA), Coster Kibonde (Urais) na Aziza Suleiman (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Makini (MAKINI), Gombo Samandito (Urais) na Husna Abdalla (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Wananchi (CUF).
Pia, Abdul Mluya (Urais) na Sadoun Khatib (Makamu wa Rais) wa Chama cha Democratic (DP), Kunje Ngombale Mwiru (Urais), Shum Abdalla (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Alliance for African Farmers (AAFP).
Wengine ni Saum Hussein Rashid (Urais) na Juma Faki (Makamu wa Rais) Chama cha United Democratic (UDP), Mwajuma Mirambo (Urais) na Mashavu Haji (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Union for Multi- party Democracy (UMD).
Wamo pia Georges Bussungu (Urais) na Ali Issa (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Tanzania Democratic Alliance (ADA- TADEA), Twalib Kadege (Urais) na Abdalla Khamisi (Makamu wa Rais) kwa Chama cha United People’s Democratic (UPDP), na Doyo Hassan (Urais) na Chausiku Mohamed (Makamu wa Rais) wa NLD.
Majalio Kyara (Urais) na Satia Bebwa (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Wilson Mulumbe (Urais) na Shoka Juma (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).
Wengine ni Haji Kha- mis (Urais) na Dk Eveline Munisi (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha (NCCR- Mageuzi), David Mwaijojele (Urais) na Masoud Abdala (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Kijamii (CCK), Salum Mwalimu (Urais) na Devotha Minja (Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) na Yustas Rwamugira (Urais) na Amana Mzee (Makamu wa Rais) kwa TLP.
Mbali na wagombea hao, pia INEC ilitoa kibali cha uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa taasisi na asasi 76 za ndani ya nchi na 12 za kimataifa.
Lakini pia katika mchakato huo wa uchaguzi INEC ilianzisha majimbo mapya manane na kubadilisha ma- jina ya majimbo 12 ya ucha- guzi yatakayotumika kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
Kwa mujibu wa INEC, Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kutakuwa na majimbo ya uchaguzi 272 yatakayo- fanya uchaguzi wa wabunge katika Jamhuri ya Muun- gano.
Aidha, kati ya majimbo hayo, 222 yapo Tanzania Bara na majimbo 50 yapo Zanzibar.
Pia, kata 3,960 zitafanya uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara katika uchaguzi huo mkuu.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com