Sh mil 250 kujenga zahanati Mwamapalala

SIMIYU: SERIKALI imetoa fedha kiasi cha Sh milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Mwamapalala iliyopo katika Kata ya Mwamapalala wilayani Itilima mkoani Simiyu.

Lengo likiwa ni kuwezesha kata hiyo kupata huduma za afya katika maeneo ya karibu na nafuu kwani hapo awali kata hiyo haikuwa na kituo cha afya pia kusogeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi hususani huduma ya afya ya uzazi na Mtoto chini ya miaka mitano.

Hayo yamebainishwa leo Machi 8,2026 mble ya Katibubwa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi alipotembelea mradi huo, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Akizingumza baada ya kukukagua mradi huo Kihongosi alisema utekeleza una ridhisha huku akimpongeza mkandarasi kwa kazi aliyoifanga kwani inaendana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali.

Pia aliagiza serikali ya Mkoa na Wilaya kwa ujumla kuhakikisha mkandarasi huyo analindwa na kuepushwa na migogoro na fitina zisizo za lazima, kwani ni muhimu kuwa na watu wanaofanya kazi kwa uadilifu kama yeye.

Kwa mujibu wa taarifa ya Muuguzi Mfawidhi wa Zahanati ya Nkololo, Bahati Clavery mradi huo umetumia zaidi ya milioni 252, ambapo Sh milioni 250 zimetoka katika serikali kuu ambayo hadi sasa imetumika Sh milioni 214 na zilizobaki ni Sh milioni 35, ili kukamilisha mradi.

Pia ilielzwa wananchi wa kijiji cha Mwamapalala walichangia Sh 2,370,000 kwa ajili ya madini ujenzi na kulipa mlinzi wa vifaa vya ujenzi wa zahanati hiyo.

Kufikia Machi 7,2026 ujenzi umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika kw aasikimia 100 ifikapo Machi 22, mwaka huu na wanatarajiw akuanza kutoa huduma katika zahanati hiyo kabla ya mwezi juni.

Ilielezwa hadi sasa wamekamilisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje, matundu manne ya vyoo ambavyo vipo katika hatua ya ukamilishaji, sehemu ya kuchomea taka, shimo la majibu na shimo la kutupa kondo la nyuma.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

  2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button