Sillo anadi vipaumbele vitatu muhimu

MANYARA: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini mkoani Manyara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Sillo, ametaja vipaumbele vitatu muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Amesema vipaumbele atakavyotekeleza kwa mwaka 2025 hadi 2030,ni upatikanaji wa maji safi na salama, ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja, upatikanaji na usambazaji wa umeme kwenye vitongoji
Amezungumza kwenye mkutano wa kampeni Kata za Qash na kijiji cha Gedamara kata ya Gallapo na kuwaomba wananchi kumpa kura yeye kama mbunge, madiwani wote wa CCM na kumpigia kura ya kishindo Dk Samia Suluhu Hassan ili kuimarisha uongozi wa CCM kwa ngazi zote.
Kwa mujibu wa Sillo, ajenda hizo ndizo msingi wa maendeleo ya wananchi kiuchumi na zote zimeorodheshwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2025-2030.
”Leo ni mgombea mpya,ninayetarajia kuendeleza utekelezaji wa Ilani pale tulipoishia,kwa wilaya nzima tulipokea fedha Bilioni 244.97,fedha hizo zimefika kwa miradi ya wananchi kupitia viongozi wawakilishi wa wananchi ambao ni Diwani,Mbunge,” ameongeza.
”Diwani anaposemea vizuri wananchi wake kupitia miradi waliyoibua hupeleka kwa Mbunge kwani ndiye anayewasemea kwa fedha zinazotoka serikali Kuu na kufikisha kwa Mheshimiwa Rais ndipo fedha zinakuja kwenye halmashauri na miradi inatekelezwa,”amebainisha Sillo.
”Nawapongeza kwa ushirikiano baina ya serikali na nyinyi wananchi pale ambapo serikali imeleta fedha na nyinyi mkaunga mkono kusukuma miradi ya maendeleo kujenga kituo cha afya,kituo cha Polisi, ujenzi wa shule na madaraja,”amesisitiza Sillo.
Pia katika kata ya Qash amewahimiza wananchi kujitokeza kuwahi vituoni kwenda kupiga kura kuchagua viongozi tarehe 29 Oktoba 2025 kwani ndio suluhisho la changamoto zinazobainishwa na wananchi mara kwa mara ikiwemo kero ya kushuka kwa bei ya mazao ya dengu na mbaazi ambapo kwa sasa huuzwa kwa shilingi mia saba kwa kilo moja jambo ambalo amesema atalifikisha serikalini.
Naye Katibu tawi la Unjeji Kata ya Qash, Fatuma Hamisi akiwakilisha wananchi wake ameomba kushughulikiwa upatikanaji wa eneo kwa ajili ya maziko (makaburi).
Aidha, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya hiyo, Solomon Mpaki, alisema Sillo ni kiongozi anayeshirikiana na vijana katika kutafuta suluhisho la changamoto zao.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Babati Vijijini, Jackson Haibey, amehimiza wananchi kuchagua “mafiga matatu” ya CCM, yaani Diwani, Mbunge na Rais, ili maendeleo yaendelee kusukumwa kwa nguvu zaidi.
Kwa upande wake mgombea udiwani kata ya Qash, (CCM) Mohamed Issa na Mgombea udiwani kata ya Gallapo (CCM) Maiko Naas waliahidi kusimamia utekelezaji wa ilani endapo watachaguliwa.
I get paid over 220 Bucks per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. the potential with this is endless…,
COPY HERE➤➤ https://work99.site