Simba wamnasa mshambuliaji kutoka Gambia

MTANDAO: SIMBA SC imetangaza kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji, Pa Omar Jobe (25) kwa kandarasi ya miaka miwili.

Taarifa hiyo imechapishwa leo na mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

Raia huyo wa Gambia amejiunga na Simba SC akitokea Zhenis FC yenye maskani yake Makao Makuu ya Nchi ya Kazakhstan, Astana.

Jobe anatarajiwa kuwa dawa ya kutibu changamoto ya ufungaji klabuni humo.

Habari Zifananazo

Back to top button