Simbu atamba mafanikio 2025

ARUSHA: Mwanariadha wa kimataifa na bingwa wa dunia wa riadha, Alphonce Simbu ameeleza furaha baada ya kurejea nchini akitokea India kushiriki mbio za km 25 za Kolkata na kushika nafasi ya pili.

Amefanikiwa kushika nafasi ya pili akitumia muda wa 1:11:56, huku mwanariadha kutoka Uganda akiibuka mshindi wa kwanza kwa muda wa 1:11:49. Mbio hizo zilifanyika nchini India Desemba 21 mwaka huu.

Simbu amesema mwaka 2025 umekuwa wa baraka kutokana na kufanya vyema katika mbio hizo kwa kumaliza nafasi ya pili, pia kuwa bingwa wa dunia na kuongeza kwake ni neema kubwa sana.

Simbu amesema kufanya vizuri ndio chanzo cha kuendelea kupata mialiko mbalimbali ya kimataifa ambapo sasa anajiandaa kushiriki mbio mwezi Februari huko Dubai na mwezi Aprili Boston Marathon nchini Marekani.

“Nashukuru sana jeshi kupitia kwa mkuu wa majeshi kwa nafasi ya kipekee ambayo ameendelea kunipatia pamoja na wachezaji wengine wa riadha kuendelea kufanya mazoezi na kushiriki mashindano mengine ya kutaifa na kimataifa kwa nafasi hiyo ndio maana tunaendelea kufanya vizuri na kujituma na tunaahidi hizi nafasi tutazitumia ili kuwakilisha taifa letu vyema,”amesema Simbu.

Simbu amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa motisha na hamasa kwa michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, BMT, Shirikisho la Riadha, kocha, wanariadha na viongozi woteΒ  katika juhudi za pamoja zinazoendelea kuzaa matunda.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. β˜…ε½‘[𝐍𝐄𝐄𝐃 ππ„πŽππ‹π„ π…πŽπ‘ 𝐏𝐀𝐑𝐓 π“πˆπŒπ„ πŽππ‹πˆππ„ π–πŽπ‘πŠ]ε½‘β˜…

    Start making cash right now… I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my befst friend earns over $19,000 a month doing this and she convinced me to try. ift was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by visiting Following Link…

    π‡πžπ«πž 𝐒𝐬 𝐈 𝐬𝐭𝐚𝐫𝐭𝐞𝐝=========> https://bs786s.blogspot.com/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button