Sudan yaangusha ndege ya Emarati

KHARTOUM,SUDAN : JESHI la anga la Sudan limeharibu ndege ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) iliyokuwa ikibeba wapiganaji mamluki kutoka Colombia, wakati ikijaribu kutua katika uwanja wa ndege unaodhibitiwa na jeshi la Sudan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na televisheni ya taifa inayoripoti kwa niaba ya jeshi, takriban watu 40 wamefariki dunia katika tukio hilo, ambalo limetajwa kuwa sehemu ya mapambano yanayoendelea kati ya jeshi la Sudan na kikundi cha waasi cha Rapid Support Forces (RSF).

Chanzo kimoja cha kijeshi, ambacho hakikutaka kutajwa jina kwa sababu za kiusalama, kiliiambia Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) kuwa ndege hiyo ya kijeshi kutoka UAE ilishambuliwa kwa bomu na kuharibiwa kabisa katika uwanja wa ndege wa Nyala, ulioko Darfur.

Hivi karibuni uwanja huo umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya anga, hasa na jeshi la Sudan, katika juhudi za kuukomboa kutoka mikononi mwa RSF ambao wamekuwa wakipambana na serikali tangu Aprili 2023. Hadi sasa, hakuna tamko lolote rasmi lililotolewa na Umoja wa Falme za Kiarabu au kundi la RSF kuhusu tukio hilo.

SOMA: RSF yaunda serikali sambamba Sudan

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button