Taasisi ya TAJU yasisitiza amani uchaguzi mkuu

DAR ES SALAAM: Taasisi ya Tanzania Jumuishi ( TAJU) imetoa wito kwa watanzania kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani huku ikihimiza watanzania kufanya ibada ya kuliombea taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

Akisoma tamko hilo mapema hii leo, Oktoba 25, 2025, Innocent Gabriel Siriwa, Katibu wa Taasisi ya TAJU, amesema kwa nia nzuri na ya kizalendo imeona iitishe hafla hiyo kuhamasisha amani.

Aidha, Innocent amesema kuwa jamii imekuwa ikisahau juu ya uwepo wa watu wenye ulemavu hivyo uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani kuelekea uchqguzi mkui ni wazi kuwa jamii inashindwa kujali uwepo wa idadi kubwa itakayoathirika ya kundi la watu walemavu.
Hata hivyo, TAJU kupitia katibu wake, Innocent Gabriel Siriwa imewaomba viongozi na wasimamizi wa uchaguzi wa mkuu wa mwezi oktoba kusimamia kwa weledi na haki ili kuendelea kuhimarisha hali ya amani iliyopo nchini.

Kwa upande wake, Emmanuel Majeshi ambaye ni Mratibu wa Dawati la Utetezi la Watu Wenye Ulemavu- THRDC, amesema kuwa amani inapotoweka kqtikq jqmii kundi linalo athirika moja kwa moja ni watu wenye ulemavu hivyo ametoa wito kwa watanzania kuilinda amani iloyopo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.




My pay at least $300/day.My co-worker says me!I’m really amazed because you really help people to have ideas how to earn money. Thank you for your ideas and I hope that you’ll achieve more and receive more blessings. I admire your Website I hope you will notice me & I hope I can also win your paypal giveaway…….. https://cashprofit7.site