Taasisi yakazia watoto kusoma sayansi nje ya nchi

SHINYANGA: TAASISI ya Global Education Link 2025 imeendelea kuhamasisha jamii na kuwashauri wazazi kuendeleza watoto wao kwenye vyuo vya mataifa ya nje vinavyotoa fani mbalimbali hasa kwa waliofaulu masomo ya sayansi.

Meneja Mkuu wa Taasisi hiyo, Regina Lema ameyasema haya leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya vyuo vikuu vya mataifa ya nje yaliyofanyika katika halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Lema amesema wapo wanamtandao wa vyuo vya mataifa ya nje zaidi ya 300 duniani hivyo kila mmoja anaweza kusoma ujuzi anaohitaji pia kutokana na mabadiliko ya tabia nchini wafugaji wanaweza kujitokeza na kujifunza namna ya kufuga kisasa, matibabu yake na utengenezaji wa vyakula vya wanyama ili kutoendelea kuharibu mazingira.

Amewashauri wachimbaji wadogo wenye vigezo na sifa kujitokeza kujisajili na kusoma fani ya utafiti wa mimba, uchimbaji salama, utunzaji wa mazingira maeneo ya uchimbaji na uchenjuaji wake na wale wenye ufaulu mzuri wataweza kufapata mpaka ufadhili wa masomo wa asilimia 50 au 70.

Jackline Sylivenus ni mhitimu wakidato cha sita kwa mwaka 2025 ambapo amesema angependa kusoma vyuo vya nje na kile atakachojifunza ataisaidia jamii na serikali katika kuwahudumia wananchi.

Mzazi kutoka kata ya Majengo Manispaa ya Kahama Aman Omary amesema nchi ya Tanzania imejaliwa kuwa na rasimali nyingi za madini na fursa kwa vijana wakajifunza namna ya kujiendeleza. kwa kuchimba kisasa bila kuharibu mazingira kwa kupata nafasi ya kusoma kozi hizo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button