Taasisi za umma zatakiwa kuimarisha mafunzo ya maadili

ARUSHA: TAASISI za Umma zimeagizwa kuweka vipaumbele kwenye mafunzo ya maadili na uwajibikaji kwa viongozi ili kuimarisha uadilifu na utawala bora mahali pa kazi.

Agizo hilo limetolewa jijini Arusha na Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimali Watu, Mosses Pesha kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Musa wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu ya maadili kwa viongozi wa umma yaliyotolewa na Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) pamoja na Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma.

Pesha amesema serikali imedhamiria kuhakikisha maadili ya utumishi wa umma yanazingatiwa ikiwemo suala zima la uwajibikaji na uadilifu mahali pa kazi na kutoa rai kwa taasisi za umma kuweka kipaumbele zaidi katika mafunzo ili kuhakikisha ufanisi wenye tija kazini unakuwepo ikiwemo uwajibikaji wa viongozi wa umma unakuwa zaidi.

“Endapo mafunzo haya mliyopata mkiyafanyia kazi tutaona tija kwa wakuu wa taasisi, menejimenti na makatibu tawala kwani maadili ni msingi mkubwa katika utumishi wa umma pamoja na uwajibikaji ”

Naye Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Usalama kutoka chuo cha IAA Dk, Adonijah Abayo akiongea kwaniaba ya Mkuu wa chuo hicho, Profesa Eliamani Sedoyeka amesema chuo hicho kwakushirikiana na Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma wameshirikiana kwa pamoja kutoa mafunzo hayo hususan katika utawala bora.

Amesema lengo ni kuwezesha wakuu wa taasisi, wenyeviti wa bodi zaidi taasisi, wakurugenzi watendaji na makatibu tawala kutoka mikoa mbalimbali wanajengewa uwezo ili kuhakikisha wanaleta tija kazini pia kuendana na kasi ya mabadililo ya teknolojia yanayokua kwa kasi. 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button