Taasisi zatakiwa kujizatiti utekelezaji wa Dira 2050

ARUSHA; WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amezitaka taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kuweka mikakati madhubuti itakayowawezesha ku jitegemea katika uendeshaji wa shughuli zao, badala ya kuendelea kutegemea bajeti ya Serikali Kuu ili kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050.

Aidha, Kapinga ameagiza Wakala wa Vipimo (WMA) ku hakikisha unawafikia wakulima walipo ili kudhibiti vitendo vya wizi wa lumbesa na mazao mengine, hatua itakayoongeza thamani katika mnyororo wa mazao na kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wakulima ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilima bila kuona tija ya kilimo chao.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Arusha wakati akifunga kikao kati ya Menejimenti ya Wizara ya Viwanda na Biashara na menejimenti za taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

Alisema kuwa endapo taasisi hizo zitaweka mipango endelevu na kuimarisha mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inayosomana, zitajiendesha kwa ufanisi zikiondokana na utegemezi wa bajeti ya Serikali Kuu na kufanya maamuzi yatakayowezesha kufikia malengo yaliyojiwekea kila taasisi.

“Hakikisheni mnaweka mi kakati imara ya kubuni vyanzo vya mapato pamoja na mifumo inayosomana ili kuondokana na utegemezi wa bajeti ya Seri kali Kuu.

“ Pia, wekeni mazingira rafiki kwa wajasiriamali ili wasa jili biashara zao kupitia mifumo ya kidijiti, badala ya kusubiri wawafuate ofisini,” alisisitiza. Vilevile, aliagiza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kuondoka ofisini na kwenda kwa wajasiriamali na wafanyabiashara ili kusajili  biashara na kampuni zao, hatua itakayoongeza ushindani katika soko.

Kwa upande wa Tume ya Ushindani (FCC), aliitaka isisubiri kupelekewa kesi pekee bali ichukue hatua mapema ikiwemo kulegeza baadhi ya masharti ili kuleta tija katika sekta ya viwanda na biashara. Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Hashil Abdallah alisema maelekezo yaliyotolewa na waziri yatafanyiwa kazi kwa

Habari Zifananazo

4 Comments

    1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

      This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

    2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

      This is what I do………………………………….. ­­­ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button