CCM yatujengea matumaini mapya

TABORA : WAKULIMA wa zao la tumbaku mkoani Tabora wameendelea kuonesha imani kubwa kwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakisema juhudi zinazofanywa na viongozi wa juu wa nchi, akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na wagombea wa nafasi mbalimbali, zimekuwa chachu ya kuimarisha kilimo hicho ambacho ni uti wa mgongo wa uchumi wa mkoa huo.

Wakulima hao walitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, uliofanyika katika Uwanja wa Kigwa B, Jimbo la Igalula, Wilaya ya Uyui mkoani humo. SOMA: Samia ahimiza kampeni zizingatie utu

Wamesema tayari serikali imeanza kutoa ruzuku ya mbolea na pembejeo kwa wakulima wa tumbaku, hatua inayowaongezea matumaini ya kupata mavuno bora na kipato kikubwa msimu ujao. Aidha, wamesema kuingia kwa makampuni makubwa ya tumbaku mkoani humo kumechangia kujengwa kwa miundombinu, kuongeza ajira kwa vijana na kukuza kipato cha wananchi pamoja na taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa wakulima hao, endapo CCM itapewa ridhaa ya kuendelea kuongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano, wanaamini mafanikio katika kilimo cha tumbaku yataongezeka na Tabora itaendelea kuwa kitovu cha uchumi kupitia zao hilo.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. Every month start earning more than $12,000 by doing very simple Online job from home.i m doing this job in my part time i have earned and received $12429 last month .I am now a good Online earner and earns enough cash for my needs. Every person can get this Online

    job pop over here this site… ­­ https://Www.Salary7.Zone

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button