TADB yajenga uelewa, kusogeza huduma kwa wakulima Kagera

KATIKA kuendeleza dhamira yake ya kuchochea maendeleo ya kilimo nchini, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeendesha semina maalum kwa wakulima wa Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera.

Semina hiyo ni jukwaa la maarifa lililowakutanisha wakulima takribani 100 kwa lengo la kupata uelewa kuhusu huduma za kifedha zinazotolewa na Benki.

SOMA: AfDB yaipiga jeki TADB usimamizi wa vihatarishi vya mabadiliko ya tabianchi

Kupitia mafunzo haya, wakulima wamepata fursa ya kujifunza kwa kina kuhusu upatikanaji wa mikopo ya kilimo, huduma za uwezeshaji wa uzalishaji, na mbinu bora za kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa kilimo.

Semina hiyo ni ushuhuda wa azma ya TADB ya kuendeleza kilimo chenye tija, jumuishi na endelevu kilimo kinachojenga maisha, jamii na uchumi wa Taifa.

Sambamba na semina hiyo, TADB inatarajia kufungua ofisi ndogo mkoani Kagera, hatua muhimu inayolenga kusogeza huduma karibu zaidi na wakulima, wafugaji, na wadau wa sekta ya kilimo.

Uwepo wa ofisi hiyo utakuwa daraja la mawasiliano na ushirikiano wa karibu kati ya Benki na jamii ya wakulima, kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa huduma, kuongeza uwajibikaji, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kupitia kilimo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button