TADB yamshukuru Rais Samia kuiwezesha kukuza mtaji

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), imemshukuru Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza katika uwezeshaji wakulima kwa kuwapatia mikopo ya Pembejeo.
Akitoa maelezo kwa Rais Samia kuhusu utendaji wa benki hiyo leo Agosti 8,2025 wakati wa maadhimisho ya kilele cha NaneNane kitaifa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Frank Nyabundege amesema mtaji wa benki hiyo umekuwa kutoka Sh bilioni 60 hadi Sh bilioni 442.
“Benki yetu itaendelea kudhamini maonesho ya Nanenane kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kwa sababu imeiwezesha kuwa na mtaji mkubwa,” amesisitiza Nyabundege.