Takukuru yachunguza miradi kubaini ubadhirifu

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Morogoro imeazisha na uchunguzi wa awali  kwenye miradi kadhaa ukiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya Tungi  kilichopo Manispaa ya Morogoro yenye thamani ya Sh milioni 720.

Mkuu wa Takukuru Mkoa, Pilly Mwakasege amesema hayo Novemba 26, 2024 wakati akitoa taarifa kwa umma ya robo mwaka ya Julai hadi Septemba 2024.

Amesema kuanzishwa kwa uchunguzi wa awali wa ujenzi wa kituo hicho ni baada ya kubainika baadhi ya milango katika jengo la Mama na mtoto haifungi, maeneo ya njia ya kupita wagonjwa hazijawekwa bati na baadhi ya majengo ambazo hayajakamilika, yameanza kuweka nyufa.

Advertisement

Mwakasege ametaja mradi mwingine ambao uchunguzi wa awali umeanzishwa ni ujenzi wa Shule ya Msingi Mtimbira katika Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi yenye madarasa 11, jengo la utawala, nyumba ya mwalimu two in one  vyoo  vya wanafunzi  na walimu yenye thamani ya Sh milioni 400.

Mradi mwingine uchunguzi wake umeanza ni wa maji katika kijiji cha Ngayaki, Wilaya ya Gairo wenye thamani ya Sh mililioni 910.6  kutokana na uwepo wa matumizi mabaya wa fedha za mradi na hali iliyosababisha viashiria vya ubadhirifu.

Mkuu wa Takukuru mkoa huyo ametaja uchuguzi mwingine umeanzishwa wa ufuatiliaji wa mradi wa ujenzi wa bweli moja ,madundu 11 ya choo na ukarabati wa nmadarasa matano katika Sekondari ya Sungaji katika Hamashauri ya wilaya ya Mvomero yenye thamani ya Sh milioni 204.2