TAKUKURU yatoa mafunzo SIDO Dodoma

Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( (PCCB) Mkoa wa Dodoma wameendesha mafunzo ya kuzuia na kupambana na rushwa na utawala bora kwa wafanyakazi wa SIDO na wajasiriamali wanaomiliki viwanda vidogo katika mtaa wa viwanda mkoani humo.
Maofisa wa PCCB waliotoa mafunzo ni Lilian Lyimo na Aksa Musabi.

Mafunzo hayo yamekuwa na lengo la kuwapa uwezo wa kutambua maafisa wa PCCB katika kupambana na vitendo vya rushwa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha utawala bora na kuongeza ufanisi katika sekta ya umma na binafsi.
Pia, wakufunzi wamesisitiza kwamba rushwa ni adui wa maendeleo na inachangia katika kuondoa fursa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.



