Tamisemi yaweka wazi gharama Uchaguzi Serikali za Mitaa

DODOMA —Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeweka wazi matumizi ya Sh bilioni 254.82 kwa ajili ya kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amesema katika taarifa ya Hotuba ya bajeti kwa mwaka 2025/26 aliyoiwasilisha Bungeni Dodoma leo kuwa kati ya fedha hizo, Sh bilioni 247.03 zilitolewa na serikali kuu, huku Sh bilioni 7.78 zikichangwa na mapato ya ndani ya halmashauri. 

Uchaguzi huu ulihusisha uteuzi wa viongozi katika ngazi za msingi, ikiwa ni pamoja na wenyeviti wa vijiji, mitaa, vitongoji, na wajumbe wa halmashauri za vijiji na kamati za mitaa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button