Tani 300,000 za sukari zinakuja- Bashe

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kwa mwaka huu Serikali itaingiza nchini zaidi ya tani 300,000 za sukari ili kukabilana na upungufu uliopo.

Amesema hadi kufikia Machi 15, 2024, tani 60,000 za sukari zitakuwa zimeingizwa nchini na hivyo kuleta unafuu kwa watumiaji.

Waziri Bashe ameyasema hayo Ikulu, Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa vyomba vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuhusu ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan huko Vatican, Norway pamoja na Addis Ababa, Ethiopia.

Waziri Bashe amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuagiza sukari kutoka nje kutokana na mashamba mengi ya miwa kuathiriwa na mvua na hivyo kuathiri uzalishaji.

Ameongeza kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ndio imeingia makubaliano na kampuni zinazoingiza sukari nchini na si wafanyabishara.

Hata hivyo, Waziri Bashe amesema tatizo lililopo sasa ni baadhi ya wafanyabiashara kuongeza bei ya sukari na mpaka sasa zaidi ya wafanyabiashara 80 wamekamatwa kwa kuongeza bei ya sukari.

Habari Zifananazo

Back to top button