Tanzania ina sababu ya kujifunza kutoka Morocco kwenye soka

MWAKA 2022 kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar, Morocco ilifika nusu fainali na kuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kufanya hivyo.

Imeweka rekodi inayoweza kudumu vizazi na vizazi na pengine, kama kuna taifa kutoka Afrika itakayoweza kuivunja rekodi hii, basi ni Morocco yenyewe.

Rekodi ya kuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kufika robo fainali ya Kombe la Dunia iliwekwa na Cameroon mwaka 1990 ilipokuja kutolewa kwenye hatua hiyo na England kwa kufungwa mabao 3-2 kwenye fainali zilizofanyika Italia.

Miaka 12 baadaye, Senegal ikawa nchi ya pili kutoka Afrika kufika hatua hiyo na kutolewa na Uturuki kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizoandaliwa kwa pamoja na Korea Kusini. Miaka minane baadaye kwe- nye fainali za Kombe la Dunia zili- zoandaliwa na Afrika Kusini, Ghana ikawa nchi ya tatu kutoka Afrika kufika robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kuliko yote katika mpira wa miguu kwa ngazi ya timu za taifa.

Kila ukiangalia Morocco, unaona ni taifa linalopiga hatua kwa kasi sana kwenye maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu na hii haiji kwa bahati mbaya, bali ni uwekezaji uliofanywa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Kutokana na uwekezaji, haishangazi kuona Morocco wakiongoza kwa kushinda mataji mengi zaidi ya michuano ya Mabingwa wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), ikishinda ubingwa huo mara tatu, mwaka 2018, 2020 na 2024.

Morocco imeshiriki mara tano fainali za michuano ya Chan; mwaka 2014, 2016, 2018, 2020 na 2024. Hii inamaanisha kwamba, katika miaka iliyoshiriki michuano hiyo, wamekosa ubingwa huo mara mbili tu.

Kwenye fainali cha Chan zilizoandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda mwaka huu, sio tu Morocco imeshinda ubingwa huo lakini pia imetoa mfungaji bora Oussama Lamlioui akifunga mabao sita, bao moja alilifunga kwa shuti kali kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Madagascar, Nairobi, Kenya lakini pia ilitoa mchezaji bora wa michuano hiyo, kiungo Mohamed Rabi Hrimat.

Kama kuna mashindano Morocco inaumiza kichwa, basi ni fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo mara ya mwisho kushinda ubingwa wake ilikuwa mwaka 1976 kwa kuifunga Guinea kwenye mchezo wa fainali.

Imeandaa mara moja tu michuano hiyo, mwaka 1988 na mwaka huu ambapo itakuwa mwenyeji tena wa michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba mpaka Februari mwakani. Pengine hii ni nafasi muhimu kwa taifa hili linalopiga hatua kwa kasi kushinda tena ubingwa wa Afcon baada ya miaka 49 iliposhinda taji hilo kwa mara ya mwisho.

Kama hawatashinda ubingwa huo kwenye Afcon wanazoziandaa wenyewe Desemba mwaka huu mpaka Februari mwakani, basi hawatakuwa na kipindi kirefu cha kusubiri kutokana na uwekezaji walioanzisha wa kuandaa timu za watoto na vijana katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Kwa nini hawatakuwa na kipindi kirefu cha kusubiri kushinda Afcon?

Jibu ni rahisi tu, ni huo uwekez- aji wao wa kipindi cha miaka 10 iliyopita ambao umeshuhudia taifa hilo likishinda taji la Chan mara tatu katika awamu tano ilizoshiriki, kufika nusu fainali za michuano hiyo iliyofanyika Ivory Coast lakini pia kufika nusu fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar mwaka 2022.

Wana dalili nyingi za kuja kufanya vizuri sio tu kwenye Afcon mwaka huu, bali hata fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico kwa sababu ni hivi karibuni, timu yao ya taifa ya chini ya umri wa miaka 20 imeshinda Kombe la Dunia la umri kwa kuifunga Argen- tina mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Santiago, Chile.

Ni wazi hiki kikosi cha chini ya umri wa miaka 20 kilichoshinda Kombe la Dunia mbele ya taifa kubwa kwenye mpira wa miguu kama Argentina, baadhi ya wachezaji wake wanaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Morocco kitakachoshiriki fainali za Afcon kwenye ardhi yao ya nyumbani baadaye mwaka huu na fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Lakini hata baadhi ya nyota walioipa nchi hii taji la Chan kama Hrimat na Lamlioui tusishangae wakijumuishwa kwenye vikosi hivyo vya Afcon na Kombe la Dunia mwakani. Hapa unapata dhamira yao ya kutawala soka la Afrika kama sio la dunia kwa ujumla kwa miaka michache sana inayokuja.

Ukiangalia mafanikio haya ya Morocco kwa umakini, unaona wazi kabisa kwa kutumia urafiki na ushirikiano uliopo baina ya shirikisho la soka la nchi hiyo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), unaona kuna kila sababu ya watalaamu wetu kwenda kujifunza juu ya uwekezaji uliofanywa na Morocco kuleta tija kwenye maendeleo ya soka ya Tanzania.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button